June 12, 2015

 
Shirika la polisi wa kimataifa Interpol limesema linasimamisha uhusiano wake na FIFA uliokuwa na lengo la kuchunguza na kukabiliana na visa vya upangwaji wa matokeo ya mechi za kandanda, kutokana na kashfa ya rushwa inayolizonga shirikisho hilo la soka duniani.
Miaka minne iliyopita FIFA iliipa interpol dolla millioni 22 kufadhili mradi ulio na lengo la kuendeleza maadili katika secta ya michezo.
Interpol inasema washirika wake wote ni sharti wadumishe na kuendeleze maadili na taratibu zinazotumiwa na interpol katika utendaji kazi wake.
FIFA imesema imesikitishwa na uamuzi huo wa Interpol na kuongeza kuwa mradi huo wa mikakati ya kuzua udandanyifu katika soka hauhusiani kwa vyovyote vile na kashfa ya madai ya rushwa dhidi ya FIFA.

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE