Meneja wa Kilimanjaro ,Pamela Kikuli akizungumza na wanahabari (hawapo)pichani.
Wanahabari wakichukua tukio.
WASHINDI wa Kilimanjaro Music Awards 2015 (KTMA) wanatarajiwa kuanikwa kesho ndani ya Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar.
Akizungumza na waandishi wa habari leo, Meneja wa Kilimanjaro, Pamela
Kikuli amesema kuwa washindi waliopatikana katika Promosheni za Bia ya
Kilimanjaro zilizofanyika nchini kote wameanza kuwasili jijini Dar es
Salaam asubuhi ya leo kushuhudia Tuzo za Kilimanjaro Tanzania Music
Awards.
“Hafla ya kukabidhi tuzo hizi inategemewa kufanyika katika Ukumbi wa
Mlimani City jijini Dar es Salaam kesho Jumamosi na jumla ya washindi 22
wanatarajiwa kuwasili leo kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania ambapo
washindi hawa wataungana na washindi wengine wanne wa hapa Dar es
Salaam,” alisema Kikuli.
Bi. Pamela aliongeza kuwa washindi hao waliochaguliwa kwa njia ya
kuponi baada wanywaji kununua bia ya Kilimanjaro kwenye Bar zilizokuwa
na Promosheni watalipiwa gharama zote za usafiri, malazi na chakula kwa
kipindi cha siku zote tatu watakazo kuwa hapa jijini.
“ Washindi watakaokuja ni kutoka katika mikoa ya Morogoro, Iringa,
Dodoma, Tanga, Mtwara, Mbeya, Kilimanjaro, Arusha, Mwanza, Kahama,
Musoma na Dar es Salaam.”
(NA DENIS MTIMA/GPL)
0 MAONI YAKO:
Post a Comment