Waziri Mkuu wa zamani na Mbunge wa Monduli, Mh. Edward Lowassa, akiwapungia mkono mamia ya wana CCM na wananchi wa Manispaa ya Lindi, waliojitokeza kwenye ofisi za chama mkoani humo Juni 17, 2015. . Mheshimiwa Lowassa ambaye amechukua fomu kuomba chama kimteue kuwani urais wa Tanzania Oktoba 25, 2015, alijizolea wana CCM 3,279.
Waziri
Mkuu wa zamani na Mbunge wa Monduli Mh. Edward Lowassa, akisalimiana
Mwana CCM huyu aliyejitokeza kumdhamini kwenye ofisi za CCM wilaya ya
Mtwara mjini, Juni 17, 2015. . Mheshimiwa Lowassa ambaye amechukua fomu
kuomba chama kimteue kuwani urais wa Tanzania Oktoba 25, 2015,
alijizolea wana CCM 3,500.
Mwana
CCM huyu wa mkoani Mtwara ambaye alikuwa miongoni mwa waliojitokeza
kumdhamini Waziri Mkuu wa zamani na Mbunge wa Monduli, Mh. Edward
Lowassa, akiomba dua iliyokuwa ikiongozwa na kaimu kadhi wa mkoa huo,
Sheikh, Kassim Kuneng’eneka, kumuombea Mh. Lowassa, baada ya kupata
wadhamini kwenye ofisi za CCM wilaya ya Mtwara Juni 17, 2015. Mheshimiwa
Lowassa alipata jumla ya wadhamini 3,500.
Waziri Mkuu wa zamani na Mbunge wa Monduli Mh. Edward Lowassa akipaya mapokezi ya WanaCCM Tanga.
Wazee wa Tanga wakimpigia Dua Mh. Lowassa.
Waziri
Mkuu wa zamani na Mbunge wa Monduli, Mh. Edward Lowassa, akikumbatiana
na Katibu Mkuu mstaafu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Balozi Juma
Mwapachu, alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa mkoa wa Tanga Juni 17,
2015, kutafuta wadhamini baada ya kuchukua fomu za kuomba CCM imteue
kuwania urais wa Tanzania kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa ,kufanyika
Oktoba 25, 2015. Mh. Lowassa ambaye awali alikuwa akitokea mikoa ya
Mtwara na Lindi, alikozoa jumla ya wana CCM waliomdhamini 6,779, pale
Tanga alivunja rekodi ya wadhamini baada ya kuwapata zaidi ya 24, 000.
9Picha zote na K-VIS MEDIA)
Waziri
Mkuu wa zamani na Mbunge wa Monduli, Mh. Edward Lowassa, akisalimiana
na Mzee Harith Bakari Mwapachu, alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa
mkoa wa Tanga Juni 17, 2015, kutafuta wadhamini baada ya kuchukua fomu
za kuomba CCM imteue kuwania urais wa Tanzania kwenye uchaguzi mkuu
unaotarajiwa ,kufanyika Oktoba 25, 2015. Mh. Lowassa ambaye awali
alikuwa akitokea mikoa ya Mtwara na Lindi, alikozoa jumla ya wana CCM
waliomdhamini 6,779, pale Tanga alivunja rekodi ya wadhamini baada ya
kuwapata zaidi ya 24, 000. (Picha zote na K-VIS MEDIA).
0 MAONI YAKO:
Post a Comment