Mtangazaji mwenye sauti nzito Bongo kupitia Clouds FM, Millard Ayo.
MTANGAZAJI mwenye sauti nzito
Bongo kutoka Clouds FM, Millard Ayo, Jumatatu iliyopita alibanwa
azungumzie uhusiano wake na warembo wenye majina makubwa nchini, Jokate
Mwegelo ‘Kidoti’, Jacqueline Wolper na Elizabeth Michael ‘Lulu’ ambapo
alimfungukia mmojammoja.
Katika mahojiano maalum na Kipindi cha
Sporah Show cha cha Clouds Tv, mtangazaji alimbana Millard akimtaka aseme ukweli kuhusu
warembo hao ambapo alianza kwa kumzungumzia Lulu kuwa hajawahi kuwa
mpenzi wake zaidi ya kumfahamu katika sanaa.
Jacqueline Wolper Massawe akiwa katika pozi.
“Kuhusu Lulu! Hapana sijawahi kabisa
kuwa na uhusiano naye. Yaani hata kuwaza sijawahi. Namfahamu kuwa ni
mwigizaji na ni mtu ambaye nimekuwa nikimfuatilia kupitia kazi zangu za
utangazaji,” alisema mtangazaji huyo staa.
Millard aliendelea kupangua, ikafika zamu ya Wolper. Alikana vikali kuwa naye hata kujuana kwao si kwa ukaribu. Alisema:
“Haa! Wolper ndiyo kabisa, nimekuwa
nikimuona na kumsikia tu, wala sikuwahi kumuwazia kwa lolote lile
isipokuwa ninamjua kama msanii wa Bongo Muvi na huwa nakutana naye kama
ninavyoweza kukutana na mtu mwingine yeyote ambaye hatujuani.”
Millard akiwa na Jokate.
Kwa upande wa Jokate, hapo alipiga kituo
kidogo na kuanza kumzungumzia kwamba, amemfahamu miaka mingi na alikuwa
akimpenda kama ‘girl friend’ wake kwani wakati anasoma alishawahi
kupanda naye daladala na wakapiga stori.
“Nampenda Jokate kwa sababu mpole,
anatoka katika familia ya wachakarikaji, hivyo nimekuwa nikimshirikisha
katika mambo yangu. Nampenda kwa sababu hiyo ila huwezi kuamini,
nilipotezana naye na baadaye tumekuja kukutana tayari yeye ni maarufu na
sikuwahi kumwambia chochote juu ya kumpenda kwangu kwa kuwa tayari ana
‘boy friend’ wake.
“Jokate naye anamjua mchumba wangu
ingawa hajawahi kumuona. Kwa sasa namchukulia kama dada yangu tu kwa
kuwa hakuna popote ambapo nimewahi kutoka naye kimapenzi hata kwa dakika
moja zaidi ya kuwasiliana naye kikazi. Mara kadhaa nimekuwa nikimtafuta
hata kama ni usiku wa manane nikiwa na jambo na huwa sisiti
kumshirikisha,” alisema Millard.
Elizabeth Michael ‘Lulu’.
Kwa upande wa Jokate baada ya
kufikishiwa taarifa ya maneno ya Millard alishangaa, akasema yeye hajui
chochote. Kwanza aliwekewa mtego kama angeuingia kwa kuambiwa Millard
amemtaja yeye kuwa ni mchumba wake, akashtuka na kusema:
“Huh! Kasema hivyo lini? Maana mimi
sijasikia lolote na siyo kweli kama ni mpenzi wangu na sijui kwa nini
kaongea hivyo. Kwa kweli sijasikia wala kuongea naye.”
Wolper yeye alipoulizwa juu ya maneno ya
Millard kwamba hawajahi kuwa karibu kwa jambo lolote zaidi ya kuonana
barabarani alishtuka:
“He! Ni kweli lakini. Hata mimi namwonaga tu. Hivi yupo kwani hapa Bongo? Sina koneksheni ya kitu chochote na yeye.”
Lulu alipotafutwa juzi, simu yake iliita kwa muda mrefu lakini hakupokea.
Kuhusu Millard na Jokate, baadhi ya
vyombo vya habari vimewahi kuripoti kuwa wako ‘klozdi’ kiasi kwamba,
maswali ni mengi kuliko majibu.
Kwenye ‘bethidei’ ya Millard
iliyofanyika Januari 26, mwaka huu nyumbani kwake, Ubungo Msewe jijini
Dar, Jokate alishiriki kwa kumpelekea keki ya ‘kumuwishi’ ambayo ilizua
utata.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment