Nyota
wa Brazil na klabu ya Barcelona Neymar hatocheza tena michuano ya Copa
America inayoendelea huko Chile baada ya kufungiwa kucheza mechi nne
kutokana na kitendo chake cha utovu wa nidhamu alichokifanya wakati
Brazi ikicheza dhidi ya Colombia mchezo ambao ulimalizika kwa Brazil
kufungwa kwa goli 1-0.
Nahodha huyo wa Brazil alioneshwa
kadi nyekundu baada ya filimbi ya mwisho ya mwamuzi kupulizwa kwenye
mchezo uliopigwa kwenye dimba la Santiago Jumatano iliyopita. Neymar
alimpiga na mpira mgongoni kwa makusudi mchezaji Pablo Armero wa
Colombia mara baada ya mwamuzi kupuliza filimbi ya mwisho kumaliza
mchezo huo.
Awali alifungiwa kucheza mechi
moja, lakini baadae shirikisho la soka la Amerika ya Kusini (South
America Football Confederation) liliongeza kifungo na faini ya dola
10,000 za Kimarekani baada ya Neymar kugundulika kuwa alimtolea maneno
machafu mwamuzi Enrique Osses raia wa Chile. Kwahiyo sasa adhabu ya
Neymar ni kifungo cha kutocheza mechi nne pamoja na faini ya dola 10,000
za kimarekani
Naye Carlos Bacca wa Colombia
amefungiwa kucheza mechi mbili na faini ya dola 5,000 za kimarekani
baada ya kuhusika kwenye vurugu zilizotokea kwenye mchezo huo ambapo
yeye alimsukuma Neymar mara baada ya kumpiga Armero kwa mpira.
Lakini
shirikisho hilo la mpira la America ya Kusini limesema, rufaa ikowazi
wa wote waliopewa adhabu na Brazil wanaweza kupinga maamuzi hayo
yaliyotolewa kabla ya mchezo wao wa mwisho wa kundi C dhidi ya Venezuela
utakaopigwa leo (Jumamosi) usiku kuamkia kesho (Jumapili).
Kwasasa Brazil wanaoongoza kundi C
na wanakutana na Venezuela ambao wametoka kupoteza mchezo wao dhidi ya
Peru lakini wakiwa wameshinda mechi yao ya ufunguzi dhidi ya Colombia.
Awali Neymar alianza kuonesha
vitendo ambavyo si vya kiungwana kwenye soka pale alipojaribu kufunga
goli kwa kutumia mkono lakini baadae ‘akambabua’ na mpira Pablo Armero
na kutaka kumpiga kichwa Jeison Murillo.
Kukosekana kwa Neymar kutamfanya
kocha wa Brazil Carlos Dunga amtumie Robinho kama mbadala wa Neymar
kwenye mechi ijayo dhidi ya Venezuela.
Dunga amekuwa akiwatumia Robinho
na Douglas Costa kwenye mazoezi ili kujaribu kutengeneza uwiano mzuri
kati yao wakati pia kiungo wa Liverpool Philipe Coutinho anatarajiwa
kuanza kwenye mchezo huo ambao utakuwa ni wa kwanza kwake tangu kuanza
kwa mashindano.
Robinho amejumuishwa kwenye
kikosi cha Dunga mwaka jana baada ya kuikosa michuano ya kombe la dunia
wakati huo kocha akiwa Scolari. Robinho ambaye alishawahi kukipiga Real
Madrid, Manchester City na AC Milan kwasasa anacheza kwenye klabu ya
Santos ya Brazil.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment