Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA wilaya ya Kilosa mkoani
Morogoro kimesema hakuna sababu wananchi kubebeshwa mizigo ya michango
isiyoisha wakati wanakabiliwa na changamoto za kukosa huduma za afya na
maji.
Wakizungumza
na wananachi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa
kanisani kata ya ruaha wilayani kilosa viongozi wa chadema wa kata,
vijiji na mitaa wamesema serikali inatumia fedha nyingi kukimbiza mwenge
nchi nzima huku ikiwaacha wananchi wakiteseka na umaskini wa kutupwa.
Pia wamewataka wananchi kutoshughulishwa na watiania wa ccm bali
wajiaandikishe ili kuwachagua viongozi watakaowaletea mabadiliko.
Naye katibu wa CHADEMA kata ya Ruaha Haji Mponda amesema CHADEMA
haitawavumilia viongozi wa serikali za mitaa walio omba ridhaa kuongoza
wananchi kupitia CHADEMA kwa lengo la kujinufaisha na kufanya ubadhilifu
wa fedha za wananchi chama kitamshughulikia bila kujali muda
aliomaliza kwenye madaraka.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment