BILA kuwataja kwa majina, msanii wa filamu
Bongo, Ruth Suka ‘Mainda’ amesema kitendo cha baadhi ya wasanii
wanaojiona wamefikia vilele vyote vya mafanikio na kuwafanyia roho mbaya
wenzao, ndiyo moja kati ya sababu kubwa zinazochangia sanaa ya uigizaji
kuporomoka. Akibwabwaja’ na mwandishi wetu hivi karibuni, Mainda ambaye kwa sasa
‘amepangua gia’ zote zenye kasi katika sanaa na kuamua kujikabidhi
madhabahuni kwa Mungu, alisema wasanii wasihangaike kumtafuta mchawi,
badala yake wajichunguze na kujitazama upya kwani wengi wao wana roho
mbaya za kutotaka wengine wapige hatua katika sanaa.
“Hakuna watu wenye roho mbaya kama wasanii wa uigizaji, kuna ambao
wanajiona wamefika vilele vya mafanikio na kwamba hakuna mwingine zaidi
yao, hivyo wamekuwa wakiwafanyia fitina wanaokuja kwa kasi kwa kuwapiga
majungu, wajiangalie upya na Mungu wa mbinguni awasaidie sana,” alisema
Mainda.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment