Wanaharakati nchini Iran
wamekasirishwa na hatua ya kuwazuia wanawake nchini humo kushabikia
mechi ya mpira wa wavu ya wanawake dhidi ya Marekani licha ya hakikisho
kuwa wangeruhusiwa.
Kumekuwa na ripoti kwamba shirikisho la
michezo nchini humo lingeruhusu idadi ndogo ya wanawake kushabikia mechi
hiyo ya ijumaa ambayo Iran ilishinda 3-0.
Lakini upinzani wa taifa hilo ulio na wahafidhina huenda ndio uliosababisha shirikisho hilo kutoruhusu hatua hiyo.
Tamaduni za taifa hilo la kiislamu zinawakataza wanawake kushiriki katika michezo ya kiume.
Hatahivyo
katika miezi ya hivi karibuni ,serikali ya rais Hassan Rouhani ilio na
msimamo wa kadri imeonekana kusikiza shiniko za wanaharakati na zile za
mashirika ya michezo ya kimataifa kupunguza vikwazo.
Shahindokht
Molaverdi,makamu wa rais wa maswala ya wanawake na yale ya familia
aliwaambia maripota wiki iliopita kwamba wanawake wataruhusiwa
kushabikia mechi ya mchezo wa mpira wa wavu upande wa wanawake dhidi ya
Marekani.
Na mapema wiki hii,shirikisho la mchezo wa mpira wa wavu
FIVB lilisema limehakikishiwa kwamba wanawake wataruhusiwa kushabikia
mechi hiyo katika uwanja wa michezo Tehran Azadi.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment