June 23, 2015

NGASSA3
Shirikisho la soka nchini, TFF, Jumanne hii limemtangaza rasmi Boniface Charles Mkwasa kuwa kocha mkuu wa Taifa Stars.
Mkwasa atasaidiwa na Hemed Morocco kutoka Zanzibar.
Taarifa hiyo imetolewa na Rais wa TFF, Jamal Malinzi alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa hoteli ya Tansoma.
Mkwasa atakuwa kocha wa timu hiyo hadi September 30.
“Kwanza niliongea na muajiri wake ambaye ni Manji kupata ruksa yake kisha tukaongea na mwalimu. Mpango tulionao na Mwalimu ni hadi Septemba 30 ingawa lolote linaweza kutokea ndani ya kipindi hicho,” alifafanua Malinzi.
“Tumempa ofa ya maslahi yote aliyokuwa analipwa kocha aliyemtangulia, yaani Nooij. Ataishi Masaki, atapewa gari na kila posho aliyokuwa anapata kocha Nooij.
Mkwasa anachukua nafasi ya kocha Maart Nooij ambaye mkataba wake ulisitishwa na TFF weekend iliyopita.

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE