Idadi ya watu waliokufa katika ajali iliyohusisha basi na treni katika
eneo la KIBAONI wilaya ya KILOSA mkoani MOROGORO imeongezeka na kufikia
WATANO baada ya dereva wa basi kufariki wakati akipatiwa matibabu Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa MOROGORO Kamishna Msaidizi MUSA MARAMBO
amesema tukio hilo limetokea baada ya basi lenye namba za usajili T837
CTM lililokuwa likienda MOROGORO kukatiza na kugonga treni.watu 25 wamejeruhiwa katika ajali hiyo baada ya gari walilokuwa
wakisafiria kugonga treni yenye nambari za usajili 88U3 lililokuwa
linatokea mkoani Dodoma kuelekea Morogoro.Mganga mkuu wa wilaya Kilosa DENNIS NGAROMBA ameelezea hali za
wawagonjwa kuwa zinatofautiana ila bado wanaendelea na matibabu lakini
pia ameeleza kuwa wanakabiliwa na changamoto kadhaa ikiwemo huduma ya
umeme hali iliyofanya baadhi ya wagonjwa kuhamishwa hospitalini hapo
MAMA JANETH MAGUFULI ATEMBELEA BANDA LA OFISI YA WAZIRI MKUU SABASABA
-
NA. MWANDISHI WETU - DAR EA SALAAM
Mke wa aliyekuwa Rais wa Tanzania, Hayati Dkt. John Pombe Magufuli, Mama
Janeth Magufuli ametembelea banda Jumuishi ...
2 hours ago
0 MAONI YAKO:
Post a Comment