July 27, 2015

DSC00633
Mgombea nafasi ya ubunge viti maalum CCM mkoa wa Singida, Wema Sepetu, akisindikizwa kwa maandamano kuelekea ukumbi wa mkutano wa kanisa la katoliki mjini Singida, kushiriki zoezi la uchaguzi wa kuchagua wana CCM wawili watakaoshika nafasi za ubunge viti maalum.
DSC00637
Mgombea nafasi ya ubunge viti maalum CCM mkoa wa Singida, Wema Sepetu, akiwa na na mgombea mwenzake Sara Mwambu, wakipokelewa kwenye lango la kuingilia kwenye  ukumbi wa mkutano wa kanisa la katoliki mjini Singida, kwa ajili ya kushiriki uchaguzi huo.Wakati Wema alishika nafasi ya nne kwa kupata kura 90, mwenzake Sara, alishika nafasi ya tano kwa kupata kura 47.
DSC00658
Mshindi wa kwanza wa ubunge wa viti maalum mkoa wa Singida, Aysharose Ndogholi Mattembe (kulia) na mshindi wa pili, Martha Mosses Mlata, waakiwashukuru wapiga kura kwa kuwapa ridhaa ya kuwa wabunge wa viti maalum mkoa wa Singida kwenye uchaguzi uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano kanisa katoliki mjini hapa.
DSC00662
Mgombea ubunge viti maalum kupitia CCM Wema Sepetu, akiwashukuru wapiga kura wa UWT mkoa wa Singida kwa waliompa kura 90 na wale pia ambao hawakumpa, kwa madai kwamba wote kwa pamoja wamemhamasisha kuanza safari yake ya kisiasa.
DSC00655
Mpiga picha wa magazeti ya Mwananchi, Mwananchi jumapili, The Citizen na Sunday citizen na mwanaspotinews@yahoo.co.uk, Leah Samike na msanii wa filamu nchini,Wema Sepetu (kulia) wakati kwenye ukumbi wa mikutano kanisa katoliki,muda mfupi kabla hawajaanza kunadi sera zao ili waweze kuchaguliwa kushika nafasi mbili za ubunge viti maalum mkoa wa Singida kupitia CCM.
DSC00649
Baadhi ya wajumbe waliohudhuria mkutano mkuu wa jumuiya ya umoja wa wanawake Tanzania  (UWT) mkoa wa Singida, walioshiriki uchaguzi mkuu wa kuchagua wabunge wawili wa viti maalum mkoa wa Singida.Mkurugenzi wa the British School ya Zanzibar, Aysharose Ndoghili Mattembe, alikuwa mshindi wa kwanza kwa kuzoa kura 318 kati ya 940 zilizopigwa.Mshindi wa pili Martha Mosses Mlata,alipata kura 325.(Picha zote na Nathaniel Limu).

Na Nathaniel Limu, Singida
MSANII  maarufu wa tasnia ya filamu nchini, Wema Isaac Sepetu, ametangaza rasmi kuwa safari yake ya kuwatumikia wakazi wa mkoa wa Singida kupitia siasa, imeanza rasmi.
Wema ametangaza azima yake hiyo, muda mfupi baada ya kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi wa waombaji  wa ubunge viti maalum CCM mkoa wa Singida uliofanyika kwenye ukumbi mkubwa wa Kanisa la mjini hapa.
Wema ambaye alishiriki kwa mara ya kwanza katika kinyang’anyiro hicho alipata kura 90 na kushika nafasi ya nne kati ya waombaji 13, wakati Mbunge wa viti maalum kwa vipindi vitatu mfululizo , Diana Mkumbo Chilolo, aliapishwa baada ya kuwa mshindi wa tatu kwa kupata kura 182.
Msanii huyo ambaye alifanya vizuri katika kujinadi, alisema amejifunza mengi na kubaini mapungufu mbalimbali yaliyochangiwa na ugeni wake katika siasa,na kwamba  kuanzia sasa anajipanga vizuri, ili aweze kufanya vizuri zaidi kwenye safari yake ya kisiasa.
“Nitumie nafasi hii kuwashukuru wale  walionipa kura 90 na wale wote walioninyima kura kwa ujumla wao,wamenipa  hamasa na ari kubwa kuanza  rasmi safari yangu ya kisiasa, Ninachoomba ni Mungu aendelee kunipa uzima, ili siku moja ndoto yangu hii, iweze kutimia”,alisema Wema huku akitabasamu.
Awali mapema Wema alipofika Ofisi ya CCM mkoa, alikuwa kivutio kikubwa na kila mwana CCM alijitahidi kupiga picha naye huku wakisahau kambi zao za uchaguzi.
Alipoanza safari ya kuelekea ukumbi wa mikutano  wa Kanisa Katoliki mahali palipofanyikia mkutano wa uchaguzi, aliandamana na kikundi cha burudani cha Ikungi, na alishangiliwa na watu wengi waliojitokeza kando kando ya barabara  kwa ajili ya kumwona.
Aidha,aadhi ya wajumbe walidai kwamba kama kujinadi kwa mgombea ingekuwa sifa pekee ya mgombea kushinda ubunge wa viti maalum, Wema angepata angeshinda nafasi hiyo.
Wamedai kwamba Wema alijinadi vizuri, kwa ufasaha mkubwa na  kwa ufupi na kuvuta hisia za wajumbe ambao walishindwa kujizuia na kuvunja kanuni kwa kumpigia makofi msanii huyo.
Chanzo: Moe Blog

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE