August 03, 2015

Hatimaye baraza kuu la Chadema limeridhia kusimama kwa muda kufanya kazi za chama aliyekuwa katibu mkuu wa chama hicho Dr Wilbrod Slaa.

Ni kishindo cha baraka za baraza kuu la Chadema likiridhia kupumzika kwa Dk Wilibroad Slaa ambaye tangu kujiunga kwa wazir mkuu mstaafu Edward Lowassa amekuwa haonekani katika vikao vyetu vya chama hicho, katika ufunguzi wa mkutano wa baraza kuu la Chadema mwenyekiti wa chama hicho taifa Freeman Mbowe amekiri kuwa licha ya Dkt Slaa kushiriki vikao mbalimbali vya chama kuhusu ujio wa lowassa, lakini ni kweli alitofautian kimtizamo na wajumbe wa kamati kuu. 

 

Aidha Freeman Mbowe amekiri pia juu ya hofu iliyokwisha kutanda kwa viongozi, wanachama na wapenzi wa chama hicho juu ya ujio wa baadhi ya vigogo kutoka ndani ya chama cha mapinduzi CCM.

 

Kwa upande wake kaimu katibu mkuu wa Chadema taifa Salum Mwalimu akizungumza katika mkutano huo pamoja na masuala mengine amewataka wanachama na wapenzi wa chama hicho kuahkikisha wanaunganisha nguvu hasa katika kipindi cha uchaguzi.

 

Miongoni mwa agenda kuu zilizojadiliwa katika baraza kuu la Chadema ni pamoja na agenda ya kupitisha ilani ya chama hicho, kupendekeza majina ya wagombea nafasi ya urais ikiwa ni pamoja na kuthibitisha mikakati na rasilimali za kuendesha kampeni za uchaguzi mkuu.

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE