Katibu Mtendaji wa Taasisi
ya Nishati Jadidifu (TAREA), Mhandisi Mathew, akiwaonesha wanahabari
Solar Power panels zinazotakiwa kuwa kwenye soko ambazo ni bora.
Ofisa Uhusiano wa TBS,
Roida Andusamile (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa
habari Makao Makuu ya Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Ubungo Dar es
Salaam leo asubuhi kuhusu shirika hilo kuanza msako mkali wa kuwabaini
wafanyabiashara wanaouza Umeme Nuru (Solar Power Panels), zilizochini ya
kiwango. Kulia ni Ofisa Viwango wa TBS, Henry Massawe na Ofisa
Udhibiti Ubora wa TBS, Ashura Katunzi.
Ofisa Udhibiti Ubora wa
TBS, Ashura Katunzi akisisitiza jambo wakati akizungumza na wanahabari.
Kutoka kushoto ni Ofisa Masoko Mwandamizi wa TBS, Gladness
Kaseka,Katibu Mtendaji wa Taasisi ya Nishati Jadidifu (TAREA), Mhandisi
Mathew Matimbwi, Ofisa Uhusiano wa TBS, Roida Andusamile.
Ofisa Viwango wa TBS, Henry Massawe akizungumza katika mkutano huo.
Wanahabari na wadau wengine wakiwa kwenye mkutano huo.
SHIRIKA la viwango Tanzania
limekuwa likifanya ukaguziwa kushtukiza wa bidhaa zilizopo sokoni na
viwandani mara kwa mara, lengo likiwa niku hakikisha kuwa bidhaa hizo
zinakidhi matakwa ya kiwango cha bidhaa husika wakatiwote.
TBS kwakushirikiana naTaasisya
NishatiJadididu (TAREA) iliamua kufanya ukaguzi wa kushtukiza kufuatia
malalamiko mengi kuhusiana na ubora waVipande vyaumemenuru katika soko
la Tanzania ilikutatuatatizo. Mnamo tarehe 23-06-2015, TBS ilifanya
ukaguzi wa Umeme Nuru (Solar Power panels) katika maeneo yafuatayo;
Keko- Mwanga, MtaawaMsimbazi, Mtaawa Congo.
TBS ilibaini baadhi ya wasambazaji walikuwa na bidhaa za umemenuru zilizo chini ya kiwangonyingizikitokeanchini China.
Jumla ya vipande vya umemenuru
1321 kutokaduka na ghala la Regal Solar Ltd vilizuiwa kuuzwa; na 164
kutokaduka la Nishati Electronics Ltd pia vilizuiwa kuuzwa baada ya
ubora wake kutiliwashaka mpaka matokeo ya maabara yatakapotoka. Na vile
vile wakaguzi walichukua sampuli kutokaduka la Keoali Power &
EquipmentsCo.Ltd.
Matokeo ya maabara yalitoka na kuonesha kuwasampuli hizo zilizochukuli wakati kama duka tajwa zimefeli.
1.Vipande vya Umeme Nuru
vinazosambazwa na Regal Solar Ltd vimefeli kufikia kiwango cha“marking
and name plate”, kwa mfano hazijaonyesha nchi zinapotengenezewa,ainaya
panel naserial namba; kipimo cha nguvu ya umeme inayotoka ni ndogo
ukilinganishanakiwango cha chini cha nguvu ya umeme inayotakiwa kutoka,
na hii ni kwa vipande vya umemenuru vilivyo na nguvu zifuatazo: 100W,
120W,70W,50W,20W,250W,30W,150W na 170W.
2.Vipandevya Umeme Nuru vya
Nishati Electronics Ltd vimefelikufikiakiwango cha “marking and name
plate”,- havijaonyesha nchi zinapotengenezwa kipimo cha nguvu ya
umemeinayotokanindogoukilinganishanakiwango cha chini cha nguvu ya umeme
inayotakiwa kutoka, hii ni kwa vipande vya umeme nuru vilivyo na nguvu
zifuatazo:
100W,80W,70W,120W,40W,200W,30W.
na kwa Vipande vya Umeme Nuru vya 120W na 200Wkiwango cha juu cha mfumo
wa nguvu ya umeme hakikubainishwa hivyo kukwamisha zoezi la upimaji.
- Keoali Power &EquipmentsCo.Ltd vipande vya umeme nuru vimeonyesha kufeli “marking and name plate- havikuoneshanchizilipotengenezwa, ainayaplate, serial
namba; havikubainisha kiasi cha juu cha mfumo wa nguvu ya umeme.
Tamko la Shirika TBS
inatoatamko kuwa zoezi hili niendelevu na iwapo msambazaji atabainika
kukiuka na kuingiza bidhaa chini ya kiwango cha Afrika Mashariki
EAS364:2005, Shirika litachukua hatua kali zakisheria.
Tunawasihi wafanyabiashara
wanaouza bidhaa hafifu za vipandevya umemenuru kuziondoa madukani mara
moja kabla Shirika halijaanza zoezi hilo.
Kushindwa kufanya hivyo
kutasababisha hatua kali za kisheria kuchukuliwa dhidi yao pindi
bidhaa hizo hafifu zitakapokutwa madukani.
Vile vile tunapenda
kuwafahamisha kuwa zoezi la kuondoa bidhaa hafifu sokoni ikiwa pamoja na
nguo za ndani,vilainishi vya mitambo,juisi (ready to drink) na mikate
ya naendelea.
Wananchi wasisite kuwasiliana nasi kupiti nanamba 0800 110 827 kwa kutumia mitandao ya TTCL na Vodacom bila gharama yoyote.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment