Asasi zisizo za serikali (Azaki) wamemtaka Rais Mteule Dr John Magufuli asimamie rasilimali za taifa ili ziwanufaishe wananchi wote na kuwatoa katika lindi la umasikini na kuleta maendeleo kwa nchi.Mkurugenzi wa Watetezi wa Haki za Binadamu Onesmo Ole Ngurumwa,
Akiongea
kwa niaba ya AZAKI, mratibu wa muungano wa asasi za kiraia za kutetea
haki za binadamu THRDC Onesmo Olengulumwa amesema kuwa katika Ilani yao
yapo maeneo yakifanyiwa kazi vizuri basi maisha ya watanzania
yatabadilika tofauti na sasa ambapo kuna upungufu wa huduma muhimu hasa
katika sekta za afya, maji, elimu na huduma za kijamii.
Olengulumwa ameongeza kuwa taifa linahitaji sera ya pamoja ya uchumi ili kuinua uchumi wa nchi ikiwa ni pamoja na usimamizi mzuri wa rasilimali za nchi ili ziwanufaishe wananchi wote.
Aidha asasi hizo za kiraia zimemtaka rais mteule Dr. Magufuli ashughulikie masuala ya haki za binadamu pamoja na kubadili mfumo uliopo ambao utatoa fursa ya kuwa na tume huru za uchaguzi na kuimarisha utawala bora.

0 MAONI YAKO:
Post a Comment