
Nyota 19 wa kikosi cha Mbeya City Fc tayari wamewasili jijini
Tanga kwa ajili ya mchezo wa ligi kuu ya soka Tanzania dhidi ya Coastal
Union uliopangwa kuchezwa kesho jumamosi kwenye uwanja wa
Mkwakwani.
Kocha wa kikosi hicho Meja Mstaafu Abdul Mingange, amesema kuwa amejiandaa vizuri kuhakikisha vijana wake wanaibuka na ushindi
siku hiyo ili kujiweka kwenye nafasi nzuri ya msimamo wa ligi
inayotarajia kushika mapumziko ya majuma kadhaa kupisha maandalizi ya
timu ya taifa.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment