
Kiongozi wa ujumbe wa waangalizi wa
uchaguzi wa Tanzania waliotoka Jumuiya ya Madola ametoa wito kwa
watakaoshindwa uchaguzini Tanzania kukubali matokeo.
Goodluck Jonathan, ambaye mwenyewe alishindwa uchaguzini na upinzani amesema uchaguzi ni kama biashara.“Kuna kushinda na kushindwa,” amenukuliwa na gazeti la The Citizen la Tanzania.

Kutokana na kupanda kwa joto la kisiasa nchini humo, Watanzania wengi wamekuwa wakifuatilia kwa karibu yanayoandikwa magazetini.
Mwandishi wa BBC Ruth Nesoba aliwapata wengi wakizingira vituo vya kuuzia magazeti Dar es Salaam kujipasha habari.
Jonathan, aliyeshindwa uchaguzini na Muhammadu Buhari mwezi Machi, alikubali matokeo upesi baada ya kushindwa na kupuuzilia mbali ushauri wa waliomtaka kupinga matokeo.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment