Najua kuna wafuatiliaji wa stori za Hekaheka kwenye show ya Leo Tena @Clouds FM… ya leo ni mwendelezo wa kisa cha siku nyingi ambacho kiliwahi kusikika kuhusu ishu ya mwanamke mmoja ambaye alimuuza mtoto wake mdogo kwa Shilingi laki mmoja.
Bibi ya mtoto huyo amesikika leo kwenye Hekaheka, amesimulia kisa chote kilivyokuwa baada ya mtoto kupatikana amesema mtoto aliumwa sana baada ya kupatikana.

Geah Habib kaongea pia na mtoto huyo ambaye kwa sasa amekua mkubwa, ana miaka nane na anasoma darasa la kwanza, jina lake anaitwa Fatuma Masai kwa sababu baada ya kuzaliwa aliuzwa laki moja kwa jamaa mmoja ambae kabila lake ni mmasai.
Hekaheka hii hapa kwenye Audio, iko stori yote kutoka kwenye show ya Leo Tena.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment