October 21, 2015

 
 Askofu wa kanisa kathoriki jimbo la morogoro Askofu Christopher  Mkude ameonya kauli ya ccmya kushinda hata kwa goli la mkono na ile ya UKAWA inayowataka wafuasi wao kulinda kura ktk uchaguzi mkuu ni kauli za kichochezi zinaweza kuchochea uvunjifu wa amani ya nchi. Mkude alikuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake ambao walikwenda kuutambulisha uongozi mpya wa chama cha waandishi wa habari mkoa wa Morogoro (Moro press) uongozi uliopo chini ya uenyekiti wa Nickson Mkilanya. "Tutashinda hata Kwa goli la mkono maana yake nini? Kwamba watashind Kwa njia yoyote Ile hata ya kuiba au maana yake nini? lakini kibaya zaidi kauli hiyo haijawahi kukemewa hata na wakubwa wake"alisema askof Mkude na kuongea Hawa wengine wanasema walinde kura kwani Hawana mawakala pale? wanataka kusema kuwa ni lazima washinde wao na jee wasiposhinda ?hizi ni kauli mbaya ambazo watanzania kwa imani zetu zote hatupaswi kuzifuata. Nchi hii yetu sote wakristo, waislam na hata wasio na dini na wasio wanasiasa tulinde amani yetu uchaguzi uishe kwa amani na kila mmoja asiwe chanzo cha kuharibu amani yetu. Uchaguzi mkuu utafanyika nchini kote siku ya Tarehe 25 jumapili ijayo

Related Posts:

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE