October 13, 2015

Uzinduzi huo umefanyika kwenye kiwanda hicho kipya kilichopo eneo la Msijute, Mtwara Vijijini mkoa wa Mtwara na kuhudhuriwa na wafanyabiashara 170 kutoka Nigeria ambao wamehudhuria sherehe hiyo kama wageni wa Alhaj Dangote.
0L7C1680
Picha – Kiwanda cha Saruji Mtwara
Ujumbe wa Dangote Group umeongozwa na Mh. Mallam Nasir Ahmad El Rufai, Gavana wa Jimbo la Kaduna ambaye pia ameiwakilisha serikali ya Nigeria ambayo imekuwa inawaasa wafanyabiashara wake kusambaza uwekezaji wao katika Bara la Afrika na hasa katika nchi zenye utulivu wa uhakika kama Tanzania.
Kiwanda hicho kipya pia kinatarajia kuajiri watu 1500 katika ajira za moja kwa moja na watu 9000 watapata ajira zisizokuwa za moja kwa moja.
Kiwanda hicho kitazalisha tani za ujazo milioni tatu kwa mwaka kimegharimu dola za kimarekani milioni 600, ikiwa ni uwekezaji mkubwa zaidi kutoka nje kuingizwa katika uchumi wa Tanzania.

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE