Kutoka
kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma za Mawasiliano, Samson Mwela,
Msemaji wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Prisca Ulomi na
mkuu wa kitengo cha sheria katika wizara hiyo, Veronica Sudayi.

Viongozi hao wakiwa makini kusikiliza na kujibu maswali yaliyokuwa yakiulizwa na wanahabari (hawapo pichani).

Waandishi wa habari wakifuatilia mkutano huo.
SERIKALI ya Tanzania kupitia
Wizara ya Sayansi Teknolojia na Mawasiliano Tanzania, leo Ijumaa imetoa
taarifa juu ya kanununi mpya za huduma za ziada za mwaka 2015 za sheria
ya mawasiliano ya kielektroniki na posta ya mwaka 2010.
Akizungumza na wanahabari jijini Dar es
Salaam, msemaji wa wizara hiyo, Prisca Ulomi, amesema kuwa hududuma za
ziada ni zile huduma za mawasiliano za kielektroniki zinazotolewa
kupitia mitandao zaidi ya huduma za msingi za mawasiliano ya kawaida.
Mlomi amefafanua kuwa, Serikali kupitia
wizara yake hiyo, ilitunga kanuni za huduma za ziada za mwaka 2015
(Value Added Services-‘VAS’ Regulation) na kuzitangaza kwenye gazeti la
serikali la Agosti 7, mwaka huu na kupewa GN. Namba 320 huku sheria hizo
zikiwa ni za mawasiliano ya kielektroniki na posta ya mwaka 2010
iliyotungwa na kuridhiwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Amesema, katika huduma hizo mtumiaji
anaweza kujiunga na kujiondoa kupata huduma hizo za ziada kwa kutumia
kanuni na sheria, endapo mtoa huduma hatozingatia taratibu zilizowekwa,
anawajibu wa kupata adhabu kwa kukiuka matakwa ya kanuni hizo.
Amefafanua kuwa, kwa kupitia kanuni hizo
za VAS, zinamtaka mtoa huduma za ziada kutoa taarifa kamili na sahihi
kuhusu huduma za ziada kwa lugha rahisi na ya uwazi ambapo ataweza kutoa
masharti na vigezo vya huduma zake ikiwemo gharama kwa njia ya
kielektroniki na kudurufu (printed and electronic formats).
Amefafanua kuwa, mtoa huduma endapo
ataamua kubadilisha huduma yake ya kielektroniki, mtumiaji atatakiwa
apatiwe taarifa kamili kuhusu masharti ya uhamaji, ikiwa ni pamoja na
mabadiliko katika utoaji wa huduma hizo na gharama endapo zitajitokeza.
Aidha kwa upande mwingine, kanuni hizo
zinamtaka mtoa huduma kuweka mfumo wa kuwezesha huduma za ziada kwa
mtumiaji kujiunga au kujiondoa ambao ni rahisi na wa uwazi kwa kutumia
teknolojia inayofaa ikiwemo ujumbe mfupi wa maneno (SMS), huduma ya
sauti au namba maalum.
Mlomi ametoa rai kwa watoa huduma za
ziada kuendelea kuzingatia kanuni na sheria katika kuwapatia wateja wao
huduma zenye ubora na viwango vinavyotakiwa na watumiaji ili kuhakikisha
wanapatiwa huduma stahiki na waliyoomba huku akitaja kuwa kanuni hizo
mpya zinapatikana kwenye tovuti ya Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na
Teknolojia ambayo ni www.mst.go.tz
Chanzo: globalpublishers.co.tz
0 MAONI YAKO:
Post a Comment