December 04, 2015

KISUTU


 


 
Watuhumiwa hao waliokaa wakiwa chini ya ulinzi wa polisi.

Watu wanane kati ya kumi na wawili waliokuwa wakishikiliwa na kuhojiwa na jeshi la Polisi kutokana na Upotevu wa makontena 329 pamoja na ukwepaji ushuru zaidi ya Billion 80 wamepandishwa kizimbani katika mahakama ya hakimu mkazi kisutu jijini dsm leo.
Watuhumiwa hao 8 wakiongozwa na kamishna wa Forodha mamlaka ya mapato Tanzania TRA Tiagi masamaki wanakabiliwa na mashtaka mawili ikiwemo kuhujumu Uchumi pamoja na upotevu wa kiasi cha shilingi Billion 12.7 na kuisababishia serikali hasara.
Imeelezwa kuwa kati ya tarehe 1 na 6 june mwaka huu katika eneo lisilofahamika washtakiwa waliidanganya serikali kwa kutoa makontena 329 bandarini na kuyapeleka katika bandari kavu ya kuhifadhiwa kontena ya Azam huku wakidai kuwa kontena hizo tayari zimelipiwa kodi kinyume kifungu cha 306 sura 16 ya mwaka 2002 .
Katika shittaka la uhujumu uchumi washtakiwa wanatuhumiwa kuisababishia serikali hasara ya mabilion ya fedha kama mapato na kodi shitaka ambalo halina dhamana kwa kuwa mahakama ya kisutu haina uwezo wa kisheria kusikiliza shauri hilo.
Hakimu Mkazi wa mahakama ya Kisutu Harun Shaidi amesema Upelelezi wa kesi hiyo bado unaendelea na kuiahirisha kesi hiyo mpaka december 17 mwaka huu huku watuhumiwa wote wanane wakipelekwa rumande
Waliopaandshwa kizimbani pamoja na Tiagi Masamaki ni Habib Hamis -Meneja huduma na Wateja -TRA, Haroun Mapande Mkuu wa Mfumo wa ICT -TRA, Raymond Adolf Luice wa TRA, mwana Dada Eliachi Mrema Afisa wa TRA Katika bandari kavu ya Azam,AShraf yusuph Khan meneja wa ICD ya Azam pamoja na Bolton Adolf Meneja Udhibiti wa TRA.

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE