Kiongozi wa
Waanglikana nchini Marekani amesema kuwa kupigwa marufuku kwa Kanisa
lake kwa kuunga mkono wapenzi wa jinsia moja kutawaletea simanzi kuu
wanandoa wa jinsia moja.
Askofu Mkuu wa Kianglikana nchini Marekani, Michael Curry, alisema hayo siku moja baada ya Waanglikana Wamarekani kupigwa marufuku kwa miaka mitatu kwa kuunga mkono wanandoa wa jinsia moja.
Askofu Curry alisema hiyo sio njia ya Mungu.
Kiongozi wa Waanglikana wote duniani, Askofu Mkuu Justin Welby, alisisitiza kuwa uamuzi huo ulijiepusha na kumeguka kwa kanisa hilo kwa sababu watu wengi wanapinga ushoga na usagaji katika ndoa.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment