January 26, 2016

Screen Shot 2016-01-26 at 5.24.13 PM 


Benki ya Walimu Tanzania (MCB) imekanusha taarifa iliyotolewa katika mitandao ya kijamii ikidai kuwa benki hiyo iko katika mchakato wa kujaza nafasi 120 za ajira.
Taarifa hiyo iliyoanza kutolewa Ijumaa ya tarehe 22, mwezi huu inadai kuwa MCB imetafuta wataalamu washauri katika sekta ya benki wanaojulikana kama Quality Service Consultants kusimamia swala zima la ajira hizo na mafunzo katika muda wa miezi sita.
Afisa Mtendaji Mkuu wa benki hiyo, Bw. Ronald Manongi amewaambia waandishi wa habari kuwa taarifa hiyo si ya kweli na yenye lengo la kupotosha umma.

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE