January 26, 2016



Maafisa nchini  wametishia kuwarejesha makwao mamia ya wahamiaji kutoka Ethiopia ambao wameingia nchini hapa kinyume na sheria wakati wakitafuta kwenda Afrika kusini. 
Tanzania imekuwa  ni kituo muhimu kwa wahamiaji , kinachotumiwa na wafanyabiashara ya kusafirisha watu kutoka Ethiopia na Somalia kwenda 
Afrika kusini na Ulaya. 
Waziri wa mambo ya ndani Ndugu Charles Kitwanga , amesema serikali imeanzisha operesheni maalum kuwakamata na kuwafikisha mahakamani Waethiopia pamoja na raia wengine wa kigeni wanaoishi ama kufanyakazi kinyume na sheria hapa mchini 
Mwezi uliopita, polisi imewakamata zaidi ya wahamiaji 40 kutoka Ethiopia, ambao wanaripotiwa kuachwa na mawakala wao ambao wamewaahidi kuwapeleka nchini Afrika kusini. Watu hao walikuwa wamejazana katika nyumba ya vyumba viwili nje kidogo ya Dar Es Salaam.

Ethiopia inakabiliwa na ukame ambao haujawahi kuonekana katika muda wa miaka 50, wakati watu zaidi ya milioni 10 hawawezi kupata chakula kwa sababu mazao yao na wanayama wamekufa.

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE