Chama cha Walimu mkoani Iringa(CWT), kimeitaka serikali mkoani Iringa
kuyavunja mabaraza ya wafanyakazi yaliyokwishamaliza muda wake na
kutendea haki kada ya ualimu kwa kuteua wajumbe wengi kutoka kada hiyo
kama kanuni za utumishi zinavyoelekeza.
Mwenyekiti
wa (CWT) mkoani humo Mwalimu Stanslaus Muhongole amesema kuwa mabaraza
hayo yaliyokwishamaliza muda yanawanyima wafanyakazi haki ya kujumuika
na hata uundwaji wa mabaraza hayo ulikiuka kanuni za utumishi kwa kuteua
wajumbe wengi kutoka kada nyingine tofauti na ualimu.
Kwa upande wake Kaimu Katibu Mkuu wa chama hicho Samuel Muhaiki
ameitaka serikali kuacha kulimbikiza madeni ya waalimu licha ya
kuendelea kusuasua katika ulipaji wa deni la waalimu hao mkoa wa Iringa
linalofikia zaidi ya shilingi milioni mia tisa
Naye mjumbe wa kamati tendaji ya CWT, Taifa anayewakilisha mkoa wa
Iringa mwalimu Pius Kiwhele ameiomba serikali kupandisha kima cha chini
cha mshahara wa walimu hadi shilingi laki sita ili kupunguza makali ya
maisha kwa waalimu
0 MAONI YAKO:
Post a Comment