Rapa wa muziki nchini Ney wa Mitego amesema kuwa moja ya mipango yake
ni kuboresha muziki wake kwa mwaka huu, ikiwa ni pamoja na kuongeza
idadi ya nyimbo atakazoachia.
Akizungumza na MTANZANIA, Ney wa Mitego alisema amekuwa akitoa nyimbo mbili au tatu kwa mwaka lakini kwa mwaka huu anataka kuachia nyimbo sita.
“Nimekuwa nikitoa nyimbo mbili kwa mwaka au tatu, kwa sasa nataka nizidi kuwapa raha mashabiki wangu kwa mambo mazuri ambayo nimewaandalia mwaka huu, nitaachia nyimbo sita badala ya tatu kama watu walivyozoea”, alisema.
Pia aliongeza kuwa mwishoni mwa mwezi huu anatarajia kuachia video yake mpya inayoenda kwa jina la ‘Saka Hela’ ambapo wimbo huo ukiwa na maadili mazuri kwa jamii na kuwaasa vijana wenzake wazidi kufanya kazi ili wawe na mafanikio.
Tayari Ney ameanza kutease wimbo mpya na ‘Saka Hela’ kwenye akaunti yake ya Instagram, na hizi ni baadhi ya post hizo;
“Mwezi huu mwishoni, Tarajia ngoma yangu mpya. #SakaHela #Team966MoneyMakers weka kwenye kumbukumbu yako hii..!!kama wewe ni shabiki wangu mwaka huu utafurahi zaidi kua my fan. Kauli mbiu yetu kwny #Team966MoneyMakers ni #SakaHela Mapenzi baadae ..!! #SakaHela
“Bahati haiji mara mbili, ukipata fursa itumie ipasavyo ..!! #SakaHela Heshima Pesa Shikamoo makelele tu! #SakaHela
“Umezaliwa mwaka gani 2005 mtoto mdogo unakula Ngano. Unapenda Ngono kumbuka kuna Gono Ukiwa Na Hamu basi Tumia #Condom ..! #SakaHela

0 MAONI YAKO:
Post a Comment