Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni imeahirisha Uchaguzi wa Umeya
uliotakiwa ufanyike leo kwa madai ya Zuio la Mahakama ya Kisutu
lililotolewa jana jioni likitaka uchaguzi huo usifanyike leo.
Akizungumza na Waandishi wa habari Mkurugenzi wa manispaa ya Kinondoni Bwana Aron Kagurumjuli amewaambia waandishi wa habari kuwa aliamua kuahirisha uchaguzi huo baada ya kupokea Zuio la Mahakama lililomfikia asubuhi ya leo likimtaka kusitisha mara moja kwa mchakato wa maandalizi ya Uchaguzi wa Umeya bila kufafanua sababu za pingamizi hilo kufika ghafla wakati wajumbe tayari walikwishafika katika eneo la uchaguzi.
Kuahirishwa kwa uchaguzi huo wa Umeya ambao ungeambatana na kuapishwa kwa Madiwani wa Wilaya ya Kinondoni kumepokelewa kwa mtazamo tofauti na upande wa Upinzani ambao unatafsiri hali hiyo na hujuma na kuahidi kutafakari uwezekano wa kulifikisha suala hilo mahakamani ili kuhakikisha haki inatendeka katika Uchaguzi huo.
Wajumbe na wagombea umeya kupitia vyama pinzani vinavyounda umoja wa katiba ya wananchi UKAWA walifika manispaa ya Kinondoni pamoja na wafuasi wao waliokuwa nje ya jengo hilo la manispaa wakishangilia lakini shangwe hizo zilizimwa na taarifa za kuahirisha uchaguzi huo.

0 MAONI YAKO:
Post a Comment