Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Rais Mstaafu wa awamu ya nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam
(Chancellor of the University of Dar es salaam).
Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue Ikulu Jijini Dar es Salaam, imeeleza kuwa uteuzi huo umeanza tarehe 17 Januari, 2016.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment