
MAKAMU wa Rais Samia Suluhu Hassan amewataka maafisa misitu kote nchini kuacha mara moja kuwahamisha wananchi wanaoishi kwenye mapori huku wakifyeka mazao yao kwa madai ya uvamizi wa hifadhi.
Kauli hiyo ameitoa wakati akiwahutubia mkutano wa hadhara mjini Geita uliofanyika katika uwanja wa shule ya msingi Kalangalala katika ziara yake ya siku mbili mkoani humo, ambapo amesema kuwa pamoja maafisa misitu nchi nzima kukaa vikao na kuelimishwa jinsi ya kuhamisha watu hao, bado baadhi yao wamekuwa wakitekeleza hatua hiyo kinyume kwa kuwanyanyasa wananchi.
Naye Mbunge wa Geita mjini Constatine Kanyasu akaitoa madai dhidi ya kampuni ya uchimbaji wa dhahabu ya Geita GGM
Pamoja na majibu ya Naibu waziri wa nishati na madini, makamu wa Rais akatoa agizo.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment