Ligi Kuu soka Tanzania bara iliendelea
kwa michezo mitano kupigwa katika viwanja tofauti, kwa upande wa Dar Es
Salaam klabu ya JKT Ruvu ilikuwa mwenyeji wa Simba katika mchezo wa 15
wa Ligi Kuu Tanzania bara msimu wa 2015/2016. Simba ilikuwa mgeni huku
huu ukiwa mchezo wao wa pili kucheza bila kuwa na kocha wao mkuu.
Huu ulikuwa mchezo unaozikutanisha timu
iliyopo nafasi ya 11 na timu iliyopo nafasi ya nafasi ya tatu, Simba
ilikuwa inahitaji point tatu ili iweze kujiweka katika nafasi nzuri ya
kushindana na Yanga wanaongoza Ligi kwa point 36 na Azam FC wanaoshika
nafasi ya pili wakiwa na point 36 sema wamezidiana magoli.
Simba walikutana na JKT Ruvu ambao
walionesha dalili ya kutaka kupata matokeo licha ya kuwa wapo nafasi ya
11, hadi kipindi cha kwanza kinamalizika hakuna timu iliokuwa
imefanikiwa kuona nyavu za mwenzake, kipindi cha pili Simba walifanya
mabadiliko na kumuingiza Hassan Kessy kuchukua nafasi ya Peter
Mwalyanza, mabadiliko ambayo yalionekana kuwa na faida.
Matokeo ya mechi nyingine za Ligi Kuu January 20
- Ndanda FC 4 – 1 Mbeya City
- Tanzania Prisons 2 – 1 Coastal Union
- Stand United 2 – 1 Toto Africans
- Mgambo JKT 1 – 2 Azam FC
Simba walifanikiwa kupata goli la kwanza
kupitia kwa Hamis Kiiza dakika ya 51, baada ya kutumia vyema nafasi ya
mkwaju wa penati aliyofanyiawa madhambi Danny Lyanga. Wakati JKT
wanatafakari namna ya kupata goli la kusawazisha, dakika ya 61 Danny Lyanga akapachika goli la pili na kuufanya mchezo umalizike kwa Simba kuibuka na ushindi wa goli 2-0.
Source:Millardayo.com
0 MAONI YAKO:
Post a Comment