February 26, 2016

 


Raia wa Switzerland Gianni Infantino amechukua mahala pake Sepp Blatter kama rais wa shirikisho la soka duniani Fifa.
katibu huyo mkuu wa Fifa alipata kura 115 katika raundi ya pili ikiwa ni kura 27 zaidi ya mpinzani wake wa karibu Sheikh Salman bin Ebrahim al-Khalifa.
Mwanamfalme Ali bin al-Hussein alikuwa wa tatu akiwa na kura nne huku Jerome Champagne akishindwa kupata hata kura moja.
Tokyo Sexwale alijiondoa kabla ya kura kuanza kupigwa mjini Zurich.


Raundi ya kwanza ya upigaji kura ilishindwa kum'baini mshindi wa moja kwa moja.
Wingi wowote wa kura[zaidi ya aslimia 50] katika raundi ya pili ya uchaguzi huo ulikuwa unaweza kumwezesha mgombea kutangazwa mshindi katika raundi ya pili.
Infantino ni wakili mwenye umri wa miaka 45 kutoka eneo la Brig jimbo la Valais nchini Switzerland ,ikiwa ni eneo lililopo chini ya maili sita kutoka nyumbani kwa Blatter.
Blatter ambaye aliliongoza shirikisho hilo tangu mwaka 1998 alijiondoa mwaka uliopita kabla ya kupigwa marufuku katika shughuli zozote za kandanda kwa kipindi cha miaka sita . 
Baada ya kutangazwa mshindi, Infantino aliwaambia wajumbe waliopiga kura kwamba hakuweza kujielezea kutokana na hisia alizokuwa nazo.
Lakini aliwaambia wajumbe kwamba ''kwa pamoja wataweza kuirudisha sura ya Fifa na heshima ya Fifa''.

Related Posts:

  • Maafisa wa kituo cha kukusanya taarifa cha TACCEO wakamatwa Wakili Imelda – Lulu Urio Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC. Chanzo:MOE BLOG Mtandao wa Asasi za Kiraia za Kuangalia chaguzi nchini jana ulipata pigo katika mwendelezo wake wa kukusanya taarifa juu ya mchakato wa… Read More
  • Obama aing'oa Burundi Mshirikishe mwenzako Image copyrightAFPImage captionMarekani imeiondoa Burundi kutoka kwenye mikataba yake ya kibiashara AGOA iliyowezesha mataifa ya Afrika kuingiza bidhaa zao katika soko la Marekani bila kulipa kodi. Mare… Read More
  • Alichokiongea DR. Magufuli baada ya kushinda nafasi ya UraiS Baada ya Rais mteule wa Tanzania, Dr. John Magufuli na Makamu wake Mama Samia Suluhu Hassan kukabidhiwa cheti na Tume ya Uchaguzi NEC, safari ilianza toka Ukumbi wa Diamond Jubilee Upanga mpaka Ofisi za CCM mta… Read More
  • Familia zaidi ya 30 Morogoro zakosa makazi Kaya 30 za kata ya Kilakala manispaa ya Morogoro hazina makazi baada ya nyumba zao kuzingirwa maji kufuatia mvua zilizo nyesha mda mfupi na kusababisha maji kuacha muelekeo baada ya kuziba mifereji ya kuyapitisha kisha kuing… Read More
  • Butiku "wazanzibar msikubali kurudia uchaguzi" Taasisi ya mwalimu Nyerere imeitaka tume ya uchaguzi ya Zanzibar ZEC kufanya kazi kwa kuzingatia katiba ya nchi na sheria na sio kutanguliza mbele maslahi binafsi ya kisiasa hatua ambayo inaweza kusababisha machafuko na umwa… Read More

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE