February 26, 2016

 Gorilla Films 152
 
 
Justine Compos





 Mtaani Randburg Gauging jijini Johannesburg nchini Afrika Kusini ndiko zilipo ofisi za Kampuni ya Gorilla Films inayomilikiwa na wapendanao Justine Compos ambaye ni direkta maarufu kwa sasa Afrika na mkewe Candice Campos.

Gorilla Films 010 
Justine Compos, Davido na wasanii wa Nigeria.
Kutokana na ubora wa video zinazotolewa na kampuni hili pamoja na kuwashika mkono wateja wake, limekuwa kimbilio kwa wasanii wengi wa Kibongo na Afrika kwa ujumla. Katika mahojiano haya ‘exclusive’ kati ya Showbiz na Justine Campos, direkta huyo amefunguka mengi kuhusu kazi zake, wasanii wa Bongo na tasnia ya muziki kwa ujumla, shuka naye;

Gorilla Films 054 
Msanii wa Marekani, Ace Hood.
Showbiz; Kampuni yako ya Gorilla Films ilianzishwa mwaka gani?
Campos; Mwaka 2002 lakini mwaka 2009 ndipo tulipoungana na Candice na kuanza kufanya kazi pamoja.
Showbiz; Nini mtazamo wako kwa wasanii wa Bongo? Wana uwezo wa kupambana katika soko la kimataifa la muziki?
Gorilla Films 068 
Campos; Kampuni yangu inajisikia poa sana kufanya kazi na wasanii kutoka Tanzania, ni watu wakarimu kuliko wengine tuliowahi kukutana nao. Kikubwa zaidi ni watu wenye malengo na juhudi, nawapa nafasi kubwa kufanya vizuri kimataifa.

Gorilla Films 122 
Joh Makin na AKA
Showbiz; Msanii gani unayempenda kuliko wote kutoka Tanzania?
Campos: Ni wengi lakini siwezi kukutajia mmojammoja.
Showbiz: Unafikiri ni nini kinawavutia wasanii wa Kitanzania kufanya kazi na kampuni yako na si kwingineko?

Gorilla Films 140 
Campos: Bila shaka ni ubora wa kazi zetu, ubunifu, kujali na uzoefu tulionao.
Showbiz: Sasa mnawasaidiaje wasanii mnaofanya nao kazi katika usambazaji wa kazi zao baada ya kuwafanyia prodaksheni kali?
Campos: Hatufanyi kazi ya usambazaji baada ya prodaksheni, labda ambacho huwa tunawasaidia wasanii wengi ni kuwashika mkono kwa kuwatambulisha kwenye vituo vikubwa vya televisheni hasa Afrika.

Gorilla Films 125 
Vanessa Mdee ‘Vee Money’
Showbiz: Inasemekama mnafanya kazi zenu vizuri sana lakini inadaiwa mnatoza mkwanja mrefu, kwani kwa video mnachukua kiasi gani?
Campos: Kila video ina gharama yake, inategemeana na idea pamoja na mahitaji yatakayohitajika kwa video hiyo.

Gorilla Films 146 
Showbiz: Kuna vigezo vyovyote vinahitajika ili msanii aweze kupiga mzigo na nyie?
Campos: Hapana, lakini kwa sasa tutahitaji zaidi kufanya kazi na wasanii tuliokwisha fanya nao kazi, wateja wapya hasa wasanii chipukizi hatuwapi nafasi sana labda ikitokea tumependa kazi yake.

Gorilla Films 069 
Msanii Sarkodie wa Ghana.
Showbiz: Wasanii wangapi wa kimataifa mmeshafanya nao kazi mpaka sasa?
Campos: Ni wengi sana, baadhi wakiwa kwenye video zao wenyewe wengine wakiwa wameshirikishwa. Kwa kuwataja tu baadhi yao ni Ace Hood kutoka Marekani, Sarkodie, Ice Prince, Wizkid, Black Coffee, Vanessa Mdee, Navy Kenzo, Diamond Platnumz, Joh Makini, Hugh Masekela, Nathan Adams, Unathi, AKA, R2Bees, Big Nelo, Oskido, Yannick, Bucie, Yemi Alade, Phyno, Runtown, Uhuru, KO Cashtime, HHP, EL, Davido, Ziyon, The Groove, Yuri Da Cunha, Sauti Sol na Ali Kiba.

Gorilla Films 152 
Justine Compos na mkewe Candice
Showbiz: Kuna tuzo yoyote mmewahi kupokea?
Kama ndiyo kwenye kipengele kipi na lini?
Campos: Ndiyo, tumepata tuzo nyingi na kuorodheshwa kwenye tuzo mbalimbali. Sina maelezo ya kutosha zaidi kwenye tuzo nyingi ila baadhi ni; Mwaka 2005 nilishindanishwa kwenye kipengele cha Direkta Bora wa Mwaka kwenye Tuzo za SAMA (South African Music Awards).
Showbiz: Unaweza kunitajia wasanii kutoka Afrika Mashariki ambao mmefanya nao kazi?

Gorilla Films 164 
Jux na video queen.
Campos: Ndiyo, baadhi yao ni Vanessa Mdee, Joh Makini, Navy Kenzo, Jux, G Nako, Ben Pol, Chegg e, Shaa, Kleyah, Diamond Platnumz na Kayumba.
Showbiz: Unaweza kuuzungumzia vipi Muziki wa Bongo Fleva ukipewa nafasi?
Campos: Nafikiri muziki wa Bongo umekuwa wa kisasa zaidi, una maudhui mazuri na kiukweli ninaufurahia tangu nimeanza kuusikia.

Gorilla Films 014 
Candice akiwa kazini.
Kitu kingine ninawapenda wasanii wa Bongo kwa sababu wana uwezo mzuri wa ‘kuperfomu’ kwenye matamasha pia kwa niaba ya kampuni yangu, nawashukuru Watanzania kwa kufuatilia kazi zetu hata wasanii wake kupenda kufanya kazi na sisi.

Related Posts:

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE