Waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Wiliam Lukuvi ameagiza kupimwa na kutolewa kwa hati za kimila kwa wananchi wa wilaya ya Mvomero sambamba na kuheshimiwa na kutambuliwa kwa hati hizo na taasisi mbalimbali za kifedha ikiwemo mabenki.
Waziri Lukuvi amesema hayo baada ya kufika wilayani Kilosa na
kupokea taarifa ya usuluhishi wa migogoro ya ardhi katika kijiji cha
Mabwegere wilayani Kilosa,kazi ambayo awali alimwagiza aliyewahi kuwa
mkuu wa mkoa wa Morogoro Steven Mashishanga kuifanya,ambapo pia
ametembelea wilaya ya Mvomero akiwa na timu ya wataalamu wa kuhakiki
mipaka ya vijiji sita vya wilaya hiyo na kupima,ambapo amekuwa ni waziri
wa tatu kutembelea wilaya hiyo ndani ya kipindi kisichozidi wiki
moja,na ametumia fursa hiyo kuzungumza na baadhi ya makundi ya wakulima
na wafugaji pamoja na viongozi,na kutoa hati milki za kimila zaidi ya
elfu saba,akitaka zitambuliwe.
Mkuu wa mkoa wa Morogoro Dr.Rajab Rutengwe amevitaka vyombo vya
usalama kutogeuka sababu ya migogoro ya ardhi katika wilaya za mkoa
huo,sambamba na kuahidi kubadili viongozi wa jeshi la polisi hususani
wilayani Mvomero ili kubadili utendaji,ambapo mkuu wa wilaya ya Mvomero
Elizabety Mkwasa akabainisha wapo baadhi ya wafugaji wanaoshiriki katika
kukuza migogoro wilayani humo ikiwemo kwa kuruhusu uingizaji wa mifugo
kiholela na kutumia watoto kuchunga bila tahadhari.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment