February 14, 2016


 
Vyama vinane vilivyoko Zanzibar vimetangaza kutokushiriki uchaguzi mkuu wa marudio unaotarajiwa kufanyika mapema Mach 20 mwaka huu.

Kwa mujibu wa taarifa iliyosainiwa na viongozi wa vyama vyote nane imesema wametangaza uamuzi huo baada ya kutokuridhishwa na maamuzi ya tume ya uchaguzi Zanzibar chini ya uenyekiti wa Jecha Salim Jecha.

 

Mwanasheria wa vyama hivyo Bw Ally Omary Juma amesema sheria No 5 ya mwaka 1992 ya bunge la Tanzania inayoruhusu uanzishwaji wa vyama vya siasa ni muhimu ikazingatiwa.

 

Licha ya CUF kutangaza mapema kutokushiriki uchaguzi huo vyama vingine vilivyotangaza kutokushiriki uchaguzi huo ni pamoja na ACT Wazalendo, Jahazi Asilia, Chauma, SAU, NRA, UPDP na UMD.

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE