Rais wa Uganda Yoweri Museveni atoa jibu kwa EU na Marekani kuhusiana na shutuma zao kwa uchaguzi wa urais nchini humo na kuwaambia kuwa hahitaji mihadhara
Yoweri Museveni atoa ujumbe kwa EU na Marekani na kuwaambia kuwa waache kuingilia siasa za Uganda.
Museveni amekuwa uongozini tangu mwaka 1986 na siku ya Jumamosi aliibuka kuwa mshindi huku mpinzani wake Kizza Besigye akikamatwa siku ya Jumapili.Ujumbe wa waangalizi wa EU ulisema kuwa shughuli za uchaguzi ulikuwa si wa haki na uadilifu.
Nchi nyingi ambazo ni wanachama wa EU zilikata misaada kwa Uganda huku Marekani ikiweka vikwazo vya visa na kusitisha mazoezi ya kikanda ya kijeshi.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment