HADITHI YA MTEGO WA PANYA
Kulikuwa na Mkulima mwenye mifugo kama ifuatavyo, alikuwa na Kuku, Mbuzi, na Ng’ombe. Mkulima aliishi na mke wake lakini alisumbuliwa sana na tatizo la Panya ndani ya Nyumba. Panya huyu alikuwa anajulikana machoni pa Kuku, Mbuzi na N’gombe.
Siku Moja Panya alikuwa akichungulia kinachoendelea ndani ya Nyumba ya Mkulima yule na alishtushwa sana kuona mkulima na mke wake wakiandaa mtego wa Panya. Panya Alipata hofu sana na akaingiwa na woga akaamua akimbie kuwapa taarifa mifugo mingine.
Akapaza sauti akitoa tahadhari “Kuna Mtego wa Panya ndani ya Nyumba, Kuna Mtego wa Panya ndani ya Nyumba!” Kuku akamjibu kwa kumuonea huruma “Najua kwamba suala hilo ni sawa na wewe kuambiwa siku yako ya kufa imefika lakini mimi hainihusu siwezi kusumbuliwa na jambo hilo”
Panya akamgeukia Mbuzi na kumwambia “Kuna Mtego wa Panya ndani ya Nyumba, Kuna Mtego wa Panya ndani ya Nyumba!” Mbuzi alimuonea huruma Panya na kumwambia “Pole sana ndugu yangu Panya lakini mimi siwezi kufanya chochote kukusaidia jua kwamba mimi nakuombea sana kwa Mungu”
Panya akamgeukia Ng’ombe na kumwambia “Kuna Mtego wa Panya ndani ya Nyumba, Kuna Mtego wa Panya ndani ya Nyumba!” Ng’ombe akamjibu “pole sana lakini sio tatizo kabisa kwangu.”
Panya akaamua kurudi kwenye Nyumba akiwa na mawazo sana na mwenye kusononeka.
Usiku ule ule sauti ikasikika Nyumba nzima, Kama sauti ya Mtego wa Panya umekamata kitu. Mke wa Mkulima alikimbia kuona kilichokamatwa. Kwenye giza, hakuweza kuona kuwa ilikuwa Nyoka mwenye sumu kali ambaye mkia wake ndio umekamatwa. Nyoka akamuuma mke wa Mkulima. Mkulima akamkimbiza hospitali na waliporudi nyumbani mke wa Mkulima akiwa na homa.
Kama ilivyo ada kwamba mgonjwa wa homa anahitaji supu nzuri ya kuku, Kwahyo Mkulima akamchinja kuku kwa ajili ya kutengeneza supu hiyo, bado mkewe hakupona kwahiyo marafiki walikuja kusaidia kumuuguza. Kuwalisha wauguzi Mkulima akamchinja Mbuzi, lakini mkewe bado hakupata nafuu. Akafariki. Watu wengi wakaja kwenye msiba wake. Ilimbidi mkulima achinje Ng’ombe ili watu wote wapate chakula.
Mwisho!
Niambie ulichojifunza, SHARE POST hii niwape stori nyingine.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment