March 28, 2016

Shambulizi la kujitoa mhanga katika bustani ya umma Pakistan
Watu 25 wameripotiwa kupoteza maisha na wengine zaidi ya 100 kujeruhiwa kufuatia shambulizi la kujitoa mhanga lililotekelezwa kwenye bustani ya umma mjini Lahore nchini Pakistan.
Afisa mkuu wa polisi wa mji wa Lahore alitoa maelezo na kuarifu kupatikana miili ya watu 25 ambayo baadaye 21 kati yao ilisafirishwa katika hospitali ya Jinnah, na mengine 4 ikasafirishwa hadi kwenye hospitali ya Sheikh Zaid.
Wengi wa watu waliopoteza maisha wamebainishwa kuwa ni watoto wadogo na wanawake.
Majeruhi 100 pia waliwezakufikishwa katika hospitali hizo mbili kuu za mji kwa ajili ya kufanyiwa matibabu.
Wengi wa majeruhi hao wanasemekana kuwa katika hali mbaya zaidi kutokana na majeraha makubwa waliyopata kwenye shambulizi hilo.

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE