March 28, 2016


harmonize kasuku - bekaboy
Staa wa Bongo fleva Rajab Abdulhan ‘Harmonize’.
Musa Mateja
Siri nje! Staa kutoka Lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB) anayejipenyeza kwa kasi kwenye Bongo Fleva, Rajab Abdulhan ‘Harmonize’ amekiri kuwa shemeji yake kwa Mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz;, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’,ndiye aliyemuunganisha na demu mkali kutoka Nairobi nchini Kenya, Huddah Monroe ‘The Boss Chick’.

vlcsnap-2015-11-30-16h52m54s213 
‘Harmonize’ akiwa na Huda.
Akizungumza ndani ya Makao Makuu ya ofisi za gazeti hili, Bamaga- Mwenge jijini Dar, wikiendi iliyopita, Harmonize alisema kuwa kwenye maisha yake hakuwahi kuwa na ndoto ya kukutana laivu na Huddah lakini bahati hiyo aliipata akiwa nchini Afrika Kusini baada ya kukutanishwa naye na Zari.
“Katika maisha yangu nilikuwa namuona tu Huddah na kumtamani ila namshukuru shemeji yangu Zari aliyenikutanisha na Huddah na kutuunganisha kuwa marafiki ambao tumekuwa tukiwasiliana utadhani tulifahamiana zaidi ya miaka hata mitano huko nyuma,” alisema Harmonize akihojiwa na Global TV Online.

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE