March 16, 2016

   

HOTUBA YA BALOZI JUMA MWAPACHU KUTANGAZA KUREJEA CCM-MIKOCHENI 16/03/2016

Ndugu zangu,

Mtakumbuka kwamba mnamo tarehe 13 Oktoba 2015, nilitangaza kuihama CCM na kurejesha kadi yangu ya uanachama kwenye ofisi ya CCM Kata ya Mikocheni. Nilitoa maelezo kwanini niliamua kujiondoa CCM (maelezo hayo pia niliyabandika katika ukurasa wangu wa facebook). 

Nilieleza kwamba CCM imepoteza mwelekeo kwa kuamua kuminyima haki ya kugombea mcha mungu Edwad Lowasa. 

Nikasema Edwad Lowasa ndiye chaguo la wana-CCM na ndiye chaguo la Watanzania. 

Nikasema nitakuwa mnafiki nikiendelea kubaki CCM huku naamini Edwad Lowasa anafaa kuwa Rais kuliko John Pombe Magufuli.

Baada ya miezi miwili ya uongozi wa Magufuli nataka niseme nilikosea sana. Nililewa mahaba ya Lowasa, nililewa ahadi ya Lowasa kunipa uwaziri wa mambo ya Nje.

Niliamini mafuriko ya Lowasa ambayo yakanifanya niamini kabisa anachukua nchi. Tulikubaliana na wenzangu kwamba wiki mbili za mwisho tuihame CCM kwa wimbi kubwa ili kuitikisa na kuitoa madarakani. Lakini baadhi wakaogopa na hadi sasa wengine wamebaki CCM na wana vyeo.

Leo natangaza kurudi CCM kwasababu nimeona kazi nzuri ya Magufuli. Nimefanya kosa kubwa katika siasa ambalo nawasihi vijana kwenye siasa wasifanye

Nilihama kwa kwasababu ya mtu (Lowassa). Nimerudi kwasababu ya mtu (Magufuli). Nataka niwaahidi kwamba CCM ikiweka mtu hovyo baada ya Magufuli, sitahama.

Usemi wa CCM kwamba Chama Kwanza, Mtu Baadaye sasa ndio nauona maana yake. Niliwalaumu CCM kwa kumuacha Lowassa lakini sikujua kwamba CCM ina uwezo wa miujiza wa kuibua jembe bora linaloitwa Magufuli.

Naomba mnisamehe kwa kulifanya jambo langu la kujitoa CCM na kurudi CCM kuwa jambo la kitaifa ukizingatia kwamba sikuwa na nafasi yoyote ya uongozi wa CCM wakati nahama na pia sijawahi kuwa hata Mjumbe wa NEC ya CCM na nilikuwa nje ya ulingo wa siasa za CCM kwa miaka 20. 

Niliamua kulifanya jambo kubwa ili kumsaidia Lowassa. Na sasa nimeamua kulifanya jambo kubwa ili Magufuli ajue sasa niko naye kwasababu sitaki shughuli zangu na za washirika wangu zikwamishwe na Serikali kwasababu tu huko nyuma niliamua kumsaidia swahiba wangu.

Naomba radhi kwa familia ya baba wa taifa mwalim Nyerere kwa kuitumia kisiasa siku aliyokufa (tar 14 Octoba) na kutumia msiba wake kutoa kauli za kisiasa zidi ya chama chake alichokiunda na ambacho hadi anakufa alikuwa mwanachama.

Wananchi wote tumuombee Magufuli na tumsaidie kwani tumepata nyerere mpya.

Related Posts:

  • Madee amemtungia wimbo huu Abdu Bonge Ilikua ni Jumamosi ya March 28 2015 ambapo zilianza kusambaa taarifa za kifo cha Miongoni mwa Waanzilishi wa kundi la Tip Top Connection Abdul Bonge,kifo ambacho inasemekana kilisababishwa na ugomvi ambao Marehemu Abdu… Read More
  • Bomoa bomoa Yaikumba Morogoro Halmashauri ya Manispaa ya morogoro ikishirikiana na mamlaka ya maji safi na maji taka mkoa wa Morogoro MORUWASA wameendesha zoezi la ubomoaji wa majengo yote yaliyopo pembezoni mwa bwawa la Mindu.Zoezi la bomoabomoa li… Read More
  • Jeshi la polisi latoa Tahadhari siku ya mkesha wa mwaka mpya   Yakiwa yamebakia masaa machache kufuatia kuuaga mwaka 2015 na kuukaribisha mwaka 2016, Jeshi la polisi nchini limetoa maelekezo ya nini kiofanyike katika kusherehekea … Read More
  • Rais Magufuli afanya uteuzi wa makatibu wakuu Rais wa Jamburi ya Muungano wa Tanzania Dokta John Pombe Magufuli amefanya uteuzi wa Makatibu wakuu na Manaibu Katibu wakuu wa wizara mbalimbali. Aidha, Rais Magufuli pia amemteua Eliakimu Maswi kuwa Kaimu Naibu Kamishna wa … Read More
  • Kamanda Suleiman Kova astaafu rasmi Leo December 31 ni siku ya mwisho kwa mwaka ,lakini pia ni siku ya mwisho kwa Kamanda wa kanda maalum ya Dar es salaam Suleiman Kova, kulitumikia jeshi la Polisi nchini kwa kuwa muda wake wa kulifanyia kazi jeshi hilo umeish… Read More

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE