Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dr Ali Mohmaed Shein
amemuapisha rasmi Balozi Seif Ali Idi kuwa makamu wa pili wa rais wa
Zanzibar baada ya kumteua juzi kushika wadhifa huo.
Hafla hiyo ya kuapishwa Balzoi Seif Ali Idi kuwa makamu wa pili wa
rais kwa kipindi cha pili mfulilizo ilifanyika Ikulu na kuhudhuriwa na
viongzoi mbalimbali wa juu wa serikali akiwemo spika mpya wa baraza la
wawakilishi Hamza Zubeir Ali, Jajai mkuu wa Zanzibar Othman Makungu na
viongzoi wengine wa SMZ.
Huu ni uteuzi wa pili uliofanywa na Dr. Shein tokea kuapishwa kuwa
rais wa Zanzibar alhamis ya wiki iliyopita ambapo tayari juzi alimteua
mwanasheria mkuu Said Hassan Said.
Balozi Seif Ali Iddi anashika wadhifa huu kwa mara ya pili mara ya
kwanza aliteuliwa Novemba mwaka 2010 na kushikilia hadi kumalizika kwa
kipindi cha miaka mitano ya kwanza ya uongozi wa awamu ya saba kufuatia
uchaguzi mkuu ulioafanyika machi 20 mwaka huu.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment