Serikali
ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imesaini hati mbili za makubaliano
na Serikali ya Japan itakayoiwezesha Tanzania kupata kiasi Yen Bilioni 6
ambazo ni sawa na Sh. Bilioni 116.4 za Kitanzania.
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kusaini hati hizo, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Servacius Likwelile alisema mkataba wa kwanza utasaidia katika kukamilisha bajeti ya Serikali ya mwaka 2016/17.
Dkt.
Likwelile alisema kuwa msaada huo unalenga kuweka mazingira rafiki ya
kwa wafanyabiashara, kuboresha masoko na kuwezesha mazingira ya
ushindani katika utengenezaji wa ajira nchini.
Mkataba
wa pili unahusu masuala ya kiufundi yatakayotumika katika kufanya
marekebisho ya mkataba uliosainiwa Octoba 20, 1966, kwa kuzingatia
sheria nyingi zimebadilika, kusainiwa kwa hati hiyo ya makubaliano
itasaidia kutabadilisha baadhi ya vifungu vyenye jina Tanzania na kuweka
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili kujumuisha pande zote mbili za
Muungano katika kutekeleza miradi ya maendeleo nchini.
Aidha,
makubaliano hayo yatasaidia kubadilisha baadhi ya vipengele vya mkataba
uliopita ikiwemo kipengele cha usambazaji wa madawa ili kuweza kukidhi
mahitaji ya sasa ya wataalamu kutoka nchini Japan kuweza kuja kufanya
kazi za kujitolea hapa nchini Tanzania.
Katibu
Mkuu Dkt. Likwelile ameishukuru Serikali ya Japan na kusisitiza kuwa
fedha hizo zitatumika kama ilivyopangwa ili kuweza kuwa na tija na
kuwaletea maendeleo Watanzania.
Naye
Balozi wa Japan nchini Tanzania Bw. Masaharu Yoshida amesema kuwa
Serikali ya Japan ina imani kuwa ushirikiano uliopo baina ya nchi hizi
mbili utasaidia kukuza maendeleo ya uchumi na kijamii.
Balozi
Yoshida amesema kuwa Serikali ya Japani inaunga mkono juhudi za
Serikali inayo ongozwa na Rais Dkt. John Magufuli katika masuala ya
viwanda na mazingira mazuri yanayovutia wawekezaji kuwekeza nchini
Tanzania.
Adha
Balozi Yoshida amesema kuwa Japan itaendelea kuwaleta vijana
wanaojitolea katika sekta ya uchumii na ya kijamii jambo limekuwa
likitekelezwa tangu mwaka 1969 ambapo hadi sasa idadi ya vijana hao wa
kujitolea imefikia zaidi ya 1500.
Katibu
Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Servacius Likwelile (kushoto)
akikisaini hati ya makubaliano kati ya Serikali ya Tanzania na Serikali
ya Japan leo jijini Dar es salaam ambao utaiwezesha Tanzania kupata
kiasi Yen Bilioni 6 ambazo ni sawa na Sh. Bilioni 116.4 za Kitanzania.
Kulia ni Balozi wa Japan nchini Tanzania Bw. Masaharu Yoshida.
Katibu
Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Servacius Likwelile akiongea na
waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya kusaini hati ya
makubaliano kati ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya Japan leo jijini
Dar es salaam ambao utaiwezesha Tanzania kupata kiasi Yen Bilioni 6
ambazo ni sawa na Sh. Bilioni 116.4 za Kitanzania.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment