JAJI mkuu wa Zanzibar Mhe. Omar Othman Makungu (wa pili kulia)
akifuatana na maafisa ya jeshi la Magereza Pemba wakati alipowatembelea
mahabusu na wafungwa katika Gereza na Wete Pemba kufahamu matatizo mbali
mbali yanayowakabili,
(Picha na Ameir Khalid).
AFISA wa kitengo cha komputa (IT) Mahakama za Pemba Mohamed Juma (kulia)
akimfahamisha jambo Jaji mkuu wa Zanzibar Mhe. Omar Othman Makungu, juu
ya utendaji kazi wa komputa za Mahakama ya Wete wakati wa ziara yake
Mahakamani hapo
AFISA Mdhamini Wizara ya Ardhi, Maji, Makaazi na Nishati Pemba Hemed
Salum Hemed akizungumzia matatizo mbali mbali yanayoikabili Mahakama ya
ardhi Wete, wakati wa ziara ya jaji mkuu katika Mahakama hiyo,
MKURUGENZI wa baraza na mji Wete Mgeni Othman aliyesimama akielezea
matatizo mbali mbali yanayoikabili Mahakama ya Mwanzo Wete, wakati jaji
mkuu wa Zanzibar alipofanya ziara Mahakamani hapo
MRAJISI wa Mahakama kuu Zanzibar Mhe. George Kazi (kulia) akichambua
madudu mbali mbali yanaliofanywa katika Mahakama ya mwanzo Wete


JAJI Mkuu wa Zanzibar mhe. Omar Othman Makungu (katikati)akiangalia moja
ya sehemu ya jengo la mahakama kuu Pemba iliyopo Chake chake baada ya
kufanyiwa matengenezo makubwa
MMOJA ya wazee wa Mahakama ya ardhi Chake chake Pemba Khamis Mzee
akielezea matatizo mbali mbali yanayoikabili mahakama hiyo katika
utendaji wake wa kazi za kila siku, wakati jaji mkuu wa Zanzibar Mhe.
Omar Othman Makungu alipofanya zaira katika mahakama hiyo
0 MAONI YAKO:
Post a Comment