Chama
cha Wafanyakazi Madereva nchini kimesema kitaitisha mgomo wa Madereva
nchi nzima endapo serikali itashindwa kutatua tatizo la ukosefu wa
Mikataba kwa madereva mpaka ifikapo Machi 31 Mwaka huu.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mwenyekiti wa Chama hicho cha
Wafanyakazi Madereva nchini Bw.Shaban Mdem,imesema Madereva hawatakuwa
tayari kufanya kazi bila kupatiwa Mikataba ambayo itawawezesha na wao
kulipa kodi kutokana na fedha wanazolipwa ili kuiwezesha nchi kupiga
hatua za kimaendeleo.
Mwenyekiti huyo pia ameitaka Serikali kupitia Jeshi la Polisi kutoa
taarifa za kifo cha aliyekuwa katibu wa chama hicho aliyefariki dunia
mapema Nov 20 Mwaka 2015.
Katika kikao hicho cha pamoja kwa Madereva wote,wametakiwa
kuhakikisha wanasimamia sheria zilizowekwa za barabarani ikiwa ni pamoja
na kuachana na tabia ya kwenda mwendo kasi kwani ndio chanzo cha uwepo
wa ajali za mara kwa mara ambazo zingeweza kuzuilika.
Madai yao ni ya msingi sana wasikilizwe!
ReplyDelete