Mmoja ya wachekeshaji bora ambao wamewahi kutokea duniani huwezi kuacha kumtaja Rowan Atkinson maarufu kwa jina la Mr. Bean ambaye kwa mujibu wa watafiti “The Observer” katika orodha iliyotolewa mwaka 2005 inamtaja Mr. Bean kuwepo katika orodha ya wachekeshaji 50 bora kwa muda wote.
Baadhi ya filamu za Mr. Bean ambazo amewahi kucheza ni Bean, Mr. Bean’s Holiday, Johnny English (2003) na Johnny English Reborn ambayo ilitoka mwaka 2011.
Mbali na umaarufu ambao Mr. Bean aliupata kupitia kazi yake ya kuchekesha lakini pia mchekeshaji huyo raia wa Uingereza ana degree ya Electrical Engineering jambo ambalo watu wengi walikuwa hawalifahamu.
Mr. Bean ambaye ni baba wa watoto wawili, alichukua degree hiyo mwaka 1975 katika Chuo Kikuu cha Newcastle na baadae kujiendeleza katika degree ya Sayansi ya Electrical Engineering katika Chuo cha The Queen’s.
Rowan Atkinson
Mr. Bean akiwa na mkewe pamoja na binti yao.

bean
Mr. Bean katika moja ya filamu zake.