March 27, 2016




Aliyekuwa Golikipa wa zamani wa Simba, Abel Dhaira amefariki Dunia
  Abel Dhaira amefariki dunia leo nchini Iceland alipokuwa akipatiwa matibabu ya ugonjwa wa kansa ya utumbo.
Golikipa huyo aliyekuwa na miaka 28 aligundulika kuwa na kansa ya tumbo mwanzoni mwa mwaka huu. 
Kifo chake kimekuja wakati ambao mkataba wake wa bima ya afya katika klabu ya  IBV Vestmanaeyjar ya Iceland – ulikuwa unamalizika. 
Dhaira alianza maisha yake ya soka katika klabu ya Walukuba  ya jijini Jinja.
Baada ya hapo alihamia Express, kisha akaenda URA kabla ya kuja kujiunga na Simba Sports Club ya Tanzania. 
Aliitumikia klabu ya IBV Vestmanaeyjar football club inayoshiriki ligi ya Iceland premier league mpaka kifo chake.  

Mungu ailaze roho yake mahala pema peponi

1 comment:

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE