Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameitakia heri timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) katika mchezo wake dhidi ya Timu ya Taifa ya Chad, utakaofanyika katika uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam, kesho tarehe 28 Machi, 2016.
Taifa
Stars itacheza mchezo huo wa marudiano, ikiwa ni wiki moja tangu
ilipocheza mchezo wa kwanza, katika Jiji la N’Djamena nchini Chad ambapo
Taifa Stars ilishinda bao 1–0.
Katika
salamu hizo Rais Magufuli amewataka wachezaji, benchi la ufundi na
viongozi wa Shirikisho la Soka hapa nchini (TFF), kutambua kuwa
watanzania wana matumaini makubwa kuwa timu yao itafanya vizuri katika
mchezo huo, ikiwa ni juhudi za kutafuta tiketi ya kufuzu kucheza
fainali za kombe la soka barani Afrika, zitakazofanyika Gabon hapo Mwaka
ujao wa 2017.
“Watanzania
wote tuiombee timu yetu ifanye vizuri ushindi wa Taifa Stars ni heshima
kwa nchi yetu na sifa muhimu kimataifa mimi naamini kama tulishinda
N’Djamena tunao uwezo wa kushinda hapo kesho” amesisitiza Rais Magufuli
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
27 Machi, 2016
0 MAONI YAKO:
Post a Comment