March 04, 2016

Mugabe: Mrithi wangu atachaguliwa kidemokrasia
Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe amekanusha madai ya kumuandaa mke wake aje kurithi kiti cha urais wa nchi hiyo na badala yake amesema kuwa, mrithi wake anapaswa kuchaguliwa kupitia njia ya demokrasia.
Akizungumza katika mahojiano aliyofanyiwa na televisheni ya serikali ya ZBC Rais Mugabe amesema kuwa, ndani ya chama cha kidemokrasia hakuna haja kwa viongozi kuteuliwa kwa ajili ya kuongoza, bali viongozi hao wanapaswa kuchaguliwa na wananchi kwa njia sahihi.
Rais Mugabe amesema kuwa, haungi mkono harakati za mkewe ndani ya chama tawala cha ZANU-PF. Rais Mugabe amezibeza taarifa zinazosema kuwa, yuko katika harakati za kumtayarisha mkewe ili aje kuwa rithi wake katika uongozi.
Rais wa Zimbabwe amesema kama ninavyomnukuu: "Kuna wengine wanasema Rais Mugabe anataka kumrirhisa kiti cha uongozi mke wake, mumeona wapi jambo kama hilo? Hata katika utamaduni wetu, wapi mmeona mke anamrithi mume wake? mwisho wa kunukuu.
Hayo yanajiri katika hali ambayo, wananchi wa Zimbabwe wanafuatilia kwa karibu afya ya kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 91 na kuna wanaoamini kwamba, kutokuwa na uwezo wa kutosha kutokana na umri na kutomuainisha mrithi wake ni jambo ambalo limeifanya nchi hiyo ikose uthabiti.
Hivi karibuni Tinomoda Chinoka, wakili wa Mahakama Kuu ya Zimbabwe alitaka kuchunguzwa hali ya afya ya rais huyo ili kuwa na uhakika kuhusiana na uongozi wake.
Mugabe amekuwa madarakani tangu Zimbabwe ilipojipatia uhuru kutoka kwa mkoloni Mwingereza hapo mwaka 1980.

Related Posts:

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE