March 31, 2016

March 31 2016 Mkurugenzi wa vipindi na uzalishaji Clouds Media Group, Ruge Mutahaba alikaa kwenye meza ya Power Breakfast Clouds FM kuongelea mambo mengi yakiwemo mafanikio ya Clouds Media Group (CMG) na kampeni zake kama Malkia wa nguvu, Baby number one na Fiesta 2016.

Tumeona sasa hivi kila baada ya miezi mitatu tuwe tunapata nafasi ya kuja kuwaambia Watazamaji wetu na wasikilizaji wetu nini tunafanya na wapenzi wetu ambao wengi tumeanza nao siku nyingi, miaka 17 sasa hivi

Mambo makubwa matatu yaliyofanywa na Clouds Media Group tangu mwaka uanze >>>Namba moja kwangu ni kuhusu Rais Magufuli kupiga simu kwenye kipindi cha 360 CloudsTV na kusema yeye ni shabiki namba moja na kupenda kinachofanywa na Watangazaji wa kipindi, namba mbili ni kampeni ya Baby namba one na ya tatu ni matokeo ya Malkia wa Nguvu‘>>>Ruge Mutahaba

Kuhusu Mikataba ya wafanyakazi ndani ya Clouds Media.. leo ni tarehe 31 kwa mimi ninavyojua kama Mkurugenzi kuna mikataba ya wafanyakazi inamalizika leo tarehe 31 lakini kwa kawaida tunatoa nafasi kwa yeyote atakayependa kuendelea aandike au aseme, kwahiyo siku ya leo ndio siku ya kusubiria>>> Ruge Mutahaba

Ruge Mutahaba aliongelea swala la Fiesta kwa kusema mwaka jana ilikuwa kuna uchaguzi kwahiyo tukaupa nafasi uchaguzi ndio maana hatukufanya Fiesta, mwaka huu fiesta itakuwepo.

Kupata yote aliyoyaongea unaweza kubonyeza play kwenye hii sauti hapa chini….

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE