Channel ten imeshuhudia watumishi wa kada mbalimbali kuitikia kwa hiari katika zoezi hilo la uhakiki na kuipongeza serikali kwa agizo hilo ambalo litapunguza udanganyifu mkubwa uliopo na fedha hizo zitasaidia kuboresha maslahi na miundombinu ya maeneo wanayoishi wafanyakazi mjini na vijijini.
Mkuu wa wilaya ya Maswa Rosemary Kirigini anayesimamia zoezi hilo amesema kwa kushirikiana na wataalamu na kamati ya ulinzi na usalama watahakikisha wanalifanya kwa umakini na hivyo watumishi watakaobainika hewa kuondolewa katika mfumo.
Tangu zoezi hilo lianze tayari wameshabaini watumishi hewa sita katika mamlaka ya maji na usafi wa mazingira Maswa ambao hawapo kazini tangu mwaka 2013 na mishahara yao bado inakuja kupitia wizara ya maji ambapo kiasi cha shilingi milioni 140 zimeonyesha kuwalipa watumishi wasio kazini.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment