
Mwanamuziki wa muziki wa Pop Adele
ameomba msamaha baada ya shabiki mmoja kujeruhiwa alipoangukiwa na
nyororo katika tamasha la Glasgow.
Nyota huyo alikuwa anaendelea
na onyesho lake katika ukumbi wa SSE Hydro siku ya ijumaa usiku wakati
nyororo hiyo ilipomuangukia mwanamke huyo aliyekuwa amekaa katika eneo
la mashabiki.Alichukuliwa na kupelekwa hospitali kama tahadhari kulingana na msemaji wa ukumbi huo.
Adele baadaye alituma ujumbe katika mtandao wake wa Tweeter akisema: Pole kwa kusikia kwamba kuna mtu alijeruhiwa katika tamasha yangu usiku.
Uchunguzi unaendelea ili kuhakikisha kisa kama hicho hakitokei tena.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment